Ijumaa 3 Julai 2026 - 03:00
Hatua ya Fedheha ya Mfalme wa Bahrain ya Kuunga Mkono Ukandamizaji Dhidi ya Waombolezaji wa Imam Hussein (as)

Hawza/ Mfalme wa Bahrain, Hamad Issa Al Khalifa, ameunga mkono hatua za serikali, mikakati ya kiusalama na sera za ukandamizaji zilizotekelezwa dhidi ya waombolezaji wa Imam Hussein (as) wakati wa maadhimisho ya Ashura ya mwaka huu.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kitengo cha tarjama cha Shirika la Habari la Hawza, Mfalme wa Bahrain, Hamad Issa Al Khalifa, ameunga mkono hatua za serikali na sera za ukandamizaji dhidi ya waombolezaji wa Imam Hussein (as) zilizotekelezwa wakati wa maadhimisho ya Ashura ya mwaka huu.

Kauli hizi zinatolewa katika wakati ambao vizuizi na ukiukwaji wa haki vinaendelea kuongezeka, huku ibada na alama za kidini za Mashia nchini Bahrain zikilengwa kwa utaratibu maalumu. Miongoni mwa hatua hizo ni kukamatwa kwa waombolezaji (madahi) na wanazuoni mashuhuri wa Kishia, kuwazuia wahubiri na waombolezaji wengi kushiriki katika majlisi za maombolezo ya Ashura baada ya kuitwa mfululizo ili kufika kwenye vyombo vya usalama na kukamatwa, pamoja na mashambulizi ya kupangwa dhidi ya alama na nembo za Ashura, sambamba na kuanzishwa kwa kampeni ya kiusalama iliyohusisha kukamatwa kwa makumi ya raia kutoka maeneo mbalimbali kwa sababu ya kuandaa na kushiriki katika maadhimisho ya Ashura.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha